Weekend iliyopita Tanzania iliingia kwenye historia baada ya mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mchezaji bora wa soka Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Pamoja na kupewa pongezi nyingi na Watanzania wakiwemo viongozi mbalimbali wa nchi..Samatta pia alionyesha kufurahishwa na mchango mkubwa aliopewa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika kuelekea kwenye mafanikio yake.
Rais mstaafu naye hakuwa nyuma katika kuonyesha furaha yake kwa mchezaji huyo na kuamua kwenda moja kwa moja katika makao makuu ya CCM kukutana na mchezaji huyo kwa lengo la kumpongeza.
Hizi ni picha za pamoja walizopiga leo January 11, 2016.
0 Comments