Bomoabomoa ilianza mwisho wa mwaka 2015 kwenye maeneo mbalimbali ambayo yalitajwa kwamba ni mabondeni, maeneo ya wazi na mengine ambayo kisheria hayakutakiwa kuwa na makazi ya watu.
Zoezi lilisimama kwa muda, baadae zikaanza kupitishwa alama za ‘X’ kwa maeneo ambayo bomoabomoa ingefatia, wapo waliofikisha kesi Mahakamani kupinga zoezi hilo… lakini ninazo Updates za hukumu ya kesi hiyo Mahakama Kuu kitengo cha ardhi Dar es Salaam.
Mahakama hiyo imeagiza zoezi la bomoabomoa kusitishwa kwa nyumba zilizoko eneo la bonde la mto Msimbazi Dar, na wamiliki wa nyumba hizo wamepewa siku 60 za kufungua kesi ya msingi Mahakamani kuhusu bomoabomoa.
#MillardAyoUPDATES: Mahakama Kuu imezuia bomoabomoa kwa muda bonde la Msimbazi Dar, waliobomolewa waruhusiwa kufungua kesi ndani ya siku 60.
— millard ayo (@millardayo)January 26, 2016
0 Comments