Header Ads Widget

Ali Chocky kutoa ngoma na Shilole


 
Ali Chocky

Stori: MUSA MATEJA

NGULI wa Muziki wa Dansi Bongo, Ali Chocky ameweka wazi nia yake ya kutaka kutoka kivingine kwa kufanya ngoma na msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

 
Shilole

Akizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Chocky alisema kwamba, tayari ameshafanya wimbo wa Bongo Fleva na Shilole kikubwa ikiwa ni kutaka kutoka kivingine zaidi kwenye soko la muziki, kwani amefikiria kupanua wigo wa muziki wake.

“Mwaka huu nimejipanga kuboresha zaidi muziki wangu na sasa nimeamua kuingia tena studio kufanya wimbo na Shilole ambao naamini nikiuachia kila mtu atakuwa na hamu ya kuusikiliza na atagundua nini ambacho nimewaza kuufanyia huu muziki,” alisema Chocky.

Post a Comment

0 Comments