Header Ads Widget

Watu 2 wajeruhiwa kwa risasi katika mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na pori la akiba Kondoa.




Mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa vijiji kumi na moja vya wilaya ya Kondoa na pori la akiba la Mkungunero umezidi kutishia amani baada ya watu wawili kudaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa wanyapori katika mashamba yaliyo pembeni mwa pori ilo ambao wamelazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Kondoa.
ITV ilifika katika hospitali ya wilaya ya Kondoa na kushuhudia majeruhi Ali Ikapu na Hamimu Salum waliyo lazwa hospiatalini hapo wakizungumza kwa shida wamesema tukio ilo limetokea wakati wananchi walipokuwa wameenda kuandaa mashamba wanayo yalima wakati wote ndipo askari wa hifadhi wakatokea kuwafukuza na kurusha risasi iliyo wajeruhi wananchi kwa madai mashambba hayo yapo ndani ya pori la Mkungunero.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kondoa Dk Ikaji Rashidi amethibitisha kuwapokea watu wawili wakiwa na majeraha katika miili yao na kwamba wamepatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

ITV ilifika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kondoa kutaka kupata msimamo wa serikali kuhusu mgogoro huo hakuweza kupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa nje ya ofisi kwa majukumu mengine lakini mwenyekiti wa halmashauri ya Kondoa Alhaji Omari kaliati akasema halmashauri inalaani tukio ilo lakini pia kuna agizo la uongozi wa juu kuhusu kumaliza mgogoro huo ambalo limepuuzwa na kuwataka wananchi wawe wavumilivu kwani baraza lijalo la madiwani litatoa tamko na maamuzi yenye tija.
CHANZO:ITV

Post a Comment

0 Comments