Vijana nchini wametakiwa kujiajiri na kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kusaidia taifa kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi zikiwemo zile zinazoweza kuzalishwa humu nchini na hivyo kuokoa fedha nyingi za kigeni hali itakayojenga na kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kutibu nguzo za umeme cha Agora Wood Treatment Plant kilichopo nje kidogo ya mji wa Iringa na kusema kuwa kama vijana wataunganisha nguvu na kuanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali taifa litaokoa fedha nyingi za kigeni kwa kuacha kuagiza bidhaa ambazo zitakuwa zinapatikana ndani ya nchi.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Agora Wood Products inayojenga kiwanda hicho Bwana Elisha Edson amesema kiwanda hicho kilichobuniwa na kuanzishwa na vijana kumi wa kitanzania kitakuwa na uwezo wa kutibu nguzo mia mbili kwa siku na kwamba ujenzi wake unakadiriwa kughalimu zaidi ya shilingi bilioni mbili huku mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Muhapa akiwataka vjina wengine kuiga mfano huo.
CREDIT:ITV
0 Comments