Bado headlines kuhusu kocha Pep Guardiola atafundisha timu gani msimu ujao zinazidi kushika kasi, najua umesikia kuwa kwa sasa Pep Guardiola atajiunga na klabu ya Machester City msimu ujao, lakini Chelsea wanatajwa kumuwania kocha huyo sambamba na klabu ya Manchester United wapinzani wa Man City.
Kwa sasa wengi wanajiuliza ni timu gani sahihi kwa Pep Guardiola anaweza fanya vizuri kulingana na falsafa yake ya ufundishaji? swali likafika kwa mchezaji wa zamani wa vilabu vya FC Barcelona, AC Milan pamoja na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho, majibu yake yalikuwa hivi “Pep ni kocha mzuri na anaweza fundisha timu yoyote duniani kwa mafanikio, Pep pia ni rafiki wa kila mtu” >>> Ronaldinho
Kuhusu swali la uchezaji wa sasa wa washambuliaji watatu FC Barcelona Neymar, Messi na Suarez unamvutia? anaweza kulinganisha na wakati wake yeye (Ronaldinho), Eto’o na Messi? “Nyakati zinabadilika, kiukweli huwezi kulinganisha hivi vizazi viwili tofauti, kila kizazi kilikuwa bora kwa wakati wake, kwa sasa wale ndio bora na Barcelona imesheheni wachezaji wazuri kwa sasa” >>> Ronaldinho
0 Comments