Kocha wa mpya wa muda wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink ambaye amejiunga kwa mara ya pili kuifundisha klabu hiyo, baada ya miaka sita toka aondoke mwishoni mwa mwaka 2009 kama kocha wa muda wa klabu hiyo, Guus Hiddink ambaye ndio ameichukua Chelsea mikononi mwa Jose Mourinho ili aiokoe isiporomoke zaidi, ameanza kwa kuwatuliza mashabiki wa Chelsea kuwa wasitegemee mabadiliko ya haraka.
Kwa miaka ya hivi karibuni Chelsea imekuwa ikifanya vizuri, hata msimu uliopita walikuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza hivyo mashabiki wake wanaweza wakatarajia mabadiliko ya haraka na kutegemea kuiona timu yao ikirudi nafasi za juu, Guus Hiddink ambaye anaamini kuwa atafanya vizuri na kuirudisha Chelsea katika nafasi nzuri amewaambia mashabiki wasitegemee kuona timu inabadilika haraka kwani inahitaji muda.
“Kama utaangalia msimu uliopita Chelsea walikuwa na mafanikio makubwa na kutwaa Kombe, najua msimu huu wana malengo kama hayo, kutwaa Ubingwa tena hususani katika Ligi Kuu Uingereza sio kitu rahisi licha ya kuwa ni lengo kuu, sio rahisi kusema tayari nipo Chelsea kesho matatizo yote yatakuwa yametatuliwa, tunahitaji muda kidogo” >>> Guus Hiddink
0 Comments