Header Ads Widget

HIVI NDIVYO MSHITAKIWA ALIVYOZIMIA BAADA YA KUSOMEWA SHITAKA LAKE JANA MAHAKAMANI,




MSHTAKIWA Hamis Malindo (30), anayekabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya, ameanguka katika chumba cha Mahakama baada ya kusomewa mashitaka yanayomkabili.


Malindo ambaye alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, alianguka baada ya Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, kumaliza kumsomea mashitaka dhidi yake, mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.

Awali akisoma mashitaka, Wakili Katuga alidai kuwa Mei 26 mwaka huu katika eneo la Gongo la Mboto, Malindo alikutwa akisafirisha gramu 12.16 za dawa za kulevya aina ya heroine.

Wakili Katuga alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Baada ya kusema hivyo, mshitakiwa alianguka chini na kuanza kutokwa na povu mdomoni, ndipo askari wakamuondoa katika chumba hicho kwenda kumpa huduma.Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 6 mwakani, itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika.

Post a Comment

0 Comments