Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya October 15 2015 katika Hifadhi ya Wanyama ya Selous, pembeni ya Mto Ruaha.
Jerry Silaa amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge Deo Filikunjombe pamoja na baba yake, Mzee William Silaa ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo >>> “Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani“— jerrysilaa
Hii ni picha ya zamani, Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
“Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr. Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS” >>> jerrysilaa
Marehemu Deo Filikunjombe na baadhi ya Wapigakura wake wa Jimbo la Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Reporter wa millardayo.com amemtafuta Jerry Silaa lakini simu yake ilipokelewa na Msaidizi wake, Fadhili Idd ambaye amesema ni kweli wanethibitishiwa kuhusu taarifa ya Msiba na wanajiandaa na taratibu nyingine kwa sasa.
RIP Marehemu Captein William Silaa & Mbunge Deo Haule Filikunjombe.
RESPECT:TZA
0 Comments