Leo tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa kupata watoto, lakini kuna wengine wanapata watoto au motto mmoja na baadae wanashindwa kupata motto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.
Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika, najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka au huaribika kabla wao hawajagundua kama walikua wajawazito.
Isipokuwa wale ambao hujua kwamba mimi nilikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 adi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zaozimeharibika au walikuwa wajawazito. Kwa maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na umekuwa haupati ujauzito lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa muda kadhaa afu hedi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA {Miscarriage}
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika adi wiki ya 20 {miezi 5} kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasa hasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo {1st trimester} lakini huweza fika adi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
i. Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba, pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito nab ado unaona damu inatoka kidogo kidogo basi ni vema kabisa kuwahi mapema kituo cha afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba {miscarriage} uwa hakutokei gafra tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.
ii. Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito, na wakati mwingine mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu nyepesi na kabra hajataamaki damu ile nzito ikaanza kutoka tena, na hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi na kunauwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema zaiti kufuata ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.
iii. Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo, kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni change na unapatwa na maumivu makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi mapema kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako usitoke au usikumbwe na tatizo hili lakutokwa na ujauzito {miscarriage}.
iv. Maumivu makali ya tumbo, wakati mwanamke anapokuwa ni mjamzito lakini wakati huwo huwo anapatwa na maumivu makali ya tumbo ya mara kwa mara yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka so ni vizuri ukawasiliana na kituo cha karibu cha afya au ukawasiliana nasi kwa matibabu zaidi.
VYANZO VYA KUHARIBIKA KWA MIMBA {Miscarriage}
Vyanzo vikubwa vya kuharibika kwa mimba ni kama vifuatavyo;
i. Chromosome abnormalities, mimba nyingi ambazo huaribika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.
ii. Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}, kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.
iii. Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.
iv. Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}, magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.
v. Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke, hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa ujauzito.
vi.Kitu kingine ni hormones {homoni} kuvurugika, kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea unbalance au kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba kuharibika hutokea.

0 Comments