Header Ads Widget

HAYA NI MANENO YA STEVE NYERERE BAADA YA KUSHINDWA KATIKA KURA ZA MAONI ZA UBUNGE CCM




.

Stori ninayokusogezea ni hii kutoka kwa msanii wa filamu Tanzania, Steve Nyerere ambaye wiki iliyopita hakufanikiwa kuwania ubunge wa jimbo la Kinondoni kutokana na kura zake kuwa chache.

Sasa leo msanii huyo amefunguka baada ya kukutana na ripota wa millardayo.com & AYO TV na kusema ‘Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu lakini niwashukuru Wananchi wa wiliaya ya Kinondoni wamenionesha upendo ambao sikutarajia kwao, la pili sikubahatika kulishika gurumo hili la kuwa kiongozi na sitaweza kukata tamaa kwasababu hivi vitu vinahitajika uvumilivu kidogo, siasa inahitaji kuwa mvumilivu na kila kitu kinachofanywa kama mwanadamu kinachotaka kupigiwa kura au kutafuta maisha ni uvumilivu unaohitajika kusonga mbele’ – Steve Nyerere


.

‘Kwasasa nipo kidogo mapumziko nikitafakari kuna yale niliyoyafanya na changamoto nilizozipata katika uchanguzi huo nimejifunza mambo mengi mengi ambayo kwangu yanatija kwa hiiyo kwangu ni changamoto kubwa sana’ – Steve Nyerere


.

RipotaTZA:Kuna taarifa tumezisikia kuwa kuna baadhi ya wasanii wameama kutoka chama cha mapinduzi na kwenda Chadema hizi taarifa zikoje?

Steve Nyerere...’Kwanza wao sio wavumilivu pili wamezaliwa na kukikuta chama cha Mapinduzi vile vile kama wasanii hapa tulipofika ni msaada mkubwa sana wa mh.Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutuonesha thamani yake kubwa kwetu ameweza kutukanwa kwaajili yetu na ameweza kututhamini, sasa leo na mimi nasikia kuwa kuna watu 15 wakiwemo wasanii wa bongo movie na wasanii wa Bongo Fleva 3 wamekiama chama cha CCM na kuhamia CHADEMA’


.

‘Mimi nasema milango iko wazi watajichuja watabaki sahihi ambao ni sisi, na mtu kama mimi sina mawazo kwasababu nimeshindwa kura za maoni niseme kwamba nihamie chama Fulani sina mawazo hayo na sitarajii kuhama mimi nimezaliwa ndani ya chama cha Mapinduzi na nitakufa ndani ya chama cha Mapinduzi na ni chama changu nakipenda kwa dhati na pia nawambia wenzangu wakishindwa huko watarudi tu kwenye chama hiki cha Mapinduzi’ -Steve Nyerere 
respect  TZA_Millardayo

Unaweza uka bonyeza Play kumsikiliza Steve Nyerere

Post a Comment

0 Comments