Kuna baadhi ya nchi duniani uvutaji wa sigara ni kitu cha kawaida na ukiangalia nchi kama Jamaica wamekuwa wamehalalisha wazi matumizi ya bangi ambayo watu wake wamekuwa wakiitumia hadharani bila tatizo.
Lakini kwa upande wa china matumizi jayo yamepigwa marufuku na sasa Serikali ya nchi hiyo imetangaza wazi kuanzia leo Juni 1, ukikutwa unavuta sigara hadharani katika ameneo ya wazi au eneo la karibu na shule ama hospitali unalipa faini.
Awali China ilipitisha sheria hiyo lakini haikuisimamia kama ambavyo imetangaza kwa sasa na sehemu zitakazokuwa zikiangaliwa zaidi ni mji mkuu wa nchi hiyo Beijing.
Ripoti ilionyesha takribani watu milioni 300 wanatumia sigara na sasa kutakuwa na faini ambapo ukikutwa unavuta hadharani utatozwa fedha ya kichina 10,000 ambayo ni sawa na dola 1600.
Wauzaji wa sigara wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kuanzia umbali wa mita 100 kutoka maeneo ambayo yamekatazwa.
0 Comments