Jina la Malala Yousafzai liliwahi kukaa kwenye vichwa vya habari vya Kimataifa mwaka 2012 kutokana na tukio la msichana huyo kupigwa risasi akiwa ndani ya basi lao la shule.
Malala alikuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, tukio la kupigwa risasi linahusishwa na ishu yake kujihusisha na harakati za kudai haki za watoto hasa wa kike kwenye suala la elimu.
Mwaka 2014 jina lake likarudi tena kwenye headlines baada ya kupewa Tuzo ya amani ya Nobel, kilichoripotiwa leo kinarudisha kumbukumbu ya tukio la kupigwa risasi mwaka 2012.
Watuhumiwa 10 ambao walikamatwa kwa kesi ya kuhusika na tukio la kumpiga risasi Malala wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Malala baada ya shambulio akiwa Hospitali.
Baada ya kupigwa risasi Malala alifanyiwa upasuaji Uingereza, baada ya hali yake kukaa sawa ameendelea na kampeni zake Kimataifa.
Malala ni mmoja ya watu wenye umri mdogo na wana rekodi kubwa.. wakati anatunukiwa Tuzo ya Nobel alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
0 Comments