Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YANGU!..
Mwanamke akiwa hajitambui( tumeficha sura kwa sababu ya maadili)
Chumba kinachodaiwa kutumika
Nyumba ya mama Seni
Mwanamke akiwa hajitambui( tumeficha sura kwa sababu ya maadili)
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Baadhi ya watu waliokamatwa na polisi
Mama Seni akipandishwa garini
Kuna stori zingine ukizisikia unaweza kufikiri ni utani ama ndoto!!
Hii ya leo imetokea mkoani Shinyanga,ambapo
Mwanamke mmoja ambaye anasadikiwa kuwa mkazi wa mtaa wa Matanda katika manispaa ya Shinyanga amefanyiwa vitendo vinavyoelezwa kuwa ni ubakaji na wanaume saba tofauti hali iliyosababisha kupoteza fahamu.
Tukio hilo limetokea leo katika mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga katika nyumba ya mama aliyefahamika kwa jina la mama Seni ambaye anajihusisha na biashara ya kuuza pombe za kienyeji.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo ni miongoni mwa wateja wa pombe za kienyeji waliofika kwa mama Seni na baada ya kulewa alianza kuvutwa na wanaume ambao pia ni wateja waliokuwa wamelewa.
Wamesema kutokana na hali hiyo ilimlazimu mwenye nyumba ambaye ndiye muuzaji wa pombe za kienyeji kumuingiza mwanamke huyo chumbani pamoja na wanaume waliokuwa wanamvuta ambao ni zaidi ya 7 .
"Huku kwenye pombe hakuna adabu kabisa,unaambiwa miongoni mwa waliombaka wamo vijana wenye nguvu ,watanashati zaidi ya saba,basi wakamfanyia ukatili ,tunaomba jeshi la polisi litende haki,waliotenda ukatili wapo na wanajulikana kabisa,tunataka wachukuliwa hatua za kisheria",mashuhuda waliongeza.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli Roja Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ametowa wito wa wananchi hasa wanawake kujiepusha na unywaji wa pombe wa kupindukia ili kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake vinavyoendelea kutokea.
Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la tukio na kushuhudia gari la polisi likiwachukua wanaume watatu wateja wa pombe za kienyeji, muuzaji wa pombe hizo aliyehafamika kwa jina la mama Seni pamoja na mwanamke aliyefanyiwa vitendo hivyo ambaye inasadikiwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu.
Na Veronica Natalis-Malunde1 blog Shinyanga
0 Comments