Marehemu Debora Timothy enzi za uhai wake.
Ni pigo la tatu sasa tangu mwezi Julai, ambapo kwa siku ya jana, kwaya ya Neema Gospel ilimpoteza Debora Timothy aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria, ambapo mpaka siku ya tarehe 28 mwezi uliopita, inaelezwa kuwa alikuwa mzima na mwenye furaha tangu hudumani na hata mazoezini.
Marehemu Debora (aliyevaa top nyeupe) akipiga makofi siku ya mazoezi.
Akiongea na mwandishi wetu asubuhi hii, mpasha habari Samuel Limbu ambae pia yeye ni kiongozi wa maombi wa kundi hilo, amesema kuwa mwanadada huyu licha ya kuwa mahari katika uimbaji wake huku akilitumikia kundi hili kwa sauti ya kwanza, lakini pia alikuwa ni mnyenyekevu, mwenye moyo wa kujituma na kumpenda Mungu.
Pichani ni Marehemu Debora (katikati) akiwa ameiwakilisha kwaya yake, kwenye mazishi ya Marehemu William Mandilindi, tarehe 14 Julai.
Aidha tunaelezwa kuwaJumapili ya tarehe tano hakuweza kabisa kufika kanisani ambapo kwa siku ya jana jioni (Jumatatu), hali ya mwanadada huyu ilizidi kuwa mbaya na ndipo wanafamilia walipo amua kumpeleka hospitali, jambo ambalo liligonga mwamba kwani njiani mgonjwa huyo aliyekuwa maututi, alifikwa na umauti.
Hiki ni kifo cha tatu tangu mwezi Julai ndani ya kundi hili, ambapo alie tangulia kufariki ni ndg. William Mandilindi, Mzee Nehemia Mahushi na sasa ni Debora Timothy jambo ambalo, Samuel Limbu amekiri kuwa ni jeraha kubwa ndani ya mioyo ya wana-kwaya waliyobaki.
Marehemu Debora Timothy
Mipango ya mazishi inaendelea huku msiba ukiwa Tabata. Marehemu hajaacha mume wala watoto. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
0 Comments