Kwa mujibu wa daily mail hizi ni picha za kwanza za mabaki ya ndege ya Air Algerie ambayo ilianguka mashariki mwa nchi ya Mali ikitokea Ouagadougou Burkina faso kuelekea Algiers Algeria.
Kwenye eneo la ajali hii iliyoua watu wote 116 waliokuwemo ndani baada ya kupoteza mawasiliano dakika 50 baada ya kupaa, kumepatikana mabaki ya ndege yenyewe pamoja na mabaki ya baadhi ya viungo vya binadamu.
Ajali hii inakamilisha hesabu ya ajali kubwa ya tatu ya ndege kutokea ndani ya kipindi cha siku saba huku nyingine zikiwa ni ajali za ndege ya Malaysia Ukraine na nyingine ya TransAsia Airways iliyotokea Taiwan na kuua watu 48.
Wafaransa 51, 27 wa Burkina Faso, Walebanon nane, Waalgeria sita, Wacanada watano na Wajerumani wanne ni miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye hii ndege huku wengine wakiwa ndugu kama inavyoonekana kwenye baadhi ya picha hapa chini.
0 Comments