Header Ads Widget

MWAROBAINI WA MAALIM SEIFU KUING'OA CCM MADARAKANI 2015 WAPATIKANA, ADAI ISMAIL JUSSA


Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, amesema kiu ya Wazanzibar ni mamlaka kamili ya dola ambapo maridhiano ya SUK hayakuwa tu kuwaunganisha Wazanzibari, lakini pia lengo lilikuwa kuyarejesha mamlaka kamili ya Zanzibar.

Jussa Ladhu ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha kujiunga na CUF Aliyekuwa mwakilishi wa CCM wa jimbo la Kiembe Samaki kabla ya kufukuzwa na CCM Agosti 26, 2013, Mansour Yusuf Himid, ambaye pia ni shemeji yake na Rais Mstaafu wa Amani Karume.

“Ingekuwa viongozi wote wa SUK wangeshirikiana mamlaka kamili ya Zanzibar ingepatikana,”alisema Jussa.

Alisema ili mamlaka kamili ya Zanzibar ipatikana tu pale Maalim Seif atakapo kuwa Rais wa Zanzibar na ana imani kuwa dawa ya hilo karibu litapatiwa ufumbuzi ambapo 2015 atakuwa Rais.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa katiba, Jussa alisema hawatakubali rasimu ambayo haitazingatia matakwa ya Wazanzibari ambayo ni muundo wa serikali tatu ili bendera ya Zanzibar ipepee katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).

Pia alisema suala la uraia na uhamiaji Zanzibar ni muhimu kwani ni kisiwa hivyo lazima kuwe na udhibiti wa wageni kutoka nje ya Zanzibar na kila Mzanzibari kuwa na paspoti ya nchi hiyo.

CHANZO: IPP MEDIA

Post a Comment

0 Comments