Kwa mujibu wa mashuhuda kadhaa waliokuwepo katika eneo la tukio tangu moto huo unatokea, Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa wana wasiwasi na hitilafu ya umeme iliyojitokeza usiku wa June 10.
Soko la Karume ni miongoni mwa masoko makubwa ya mitumba yanayotumiwa na wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam na maeneo jirani kutokana na urahisi wa bei wa bidhaa zinazopatikana hapo.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa asubuhi ya leo baada ya tukio hilo ikionyesha madhara makubwa yaliyotokea baada ya ajali hiyo mbaya.
0 Comments