Header Ads Widget

UNAAMBIWA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI POLISI TABORA WAKAMATWA



Suzan S. Kaganda -ACP



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA






Anwani ya Simu: POLISI TABORA
Fax: 026 – 2605489
Nambari za Simu: 026 – 2605478
Unapojibu tafadhali taja.



Ofisi ya:-
KAMANDA WA POLISI MKOA,
S.L.P. 23,
TABORA.





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 26/05/2014.


Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linaendelea na Operesheni katika wilaya zote za mkoa wa Tabora. Ambapo kufuatia operesheni hiyo tumefanikiwa kukamata :-
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI:
Katika mwendelezo wa upelelezi wa matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha hapa mkoani Tabora walikamatwa watuhumiwa saba waliohusika na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha na mauaji ya askari Na.F.5179 Pc Jumanne na G.3388 Pc Shabani huko Usoke Wilaya ya Urambo.Watuhumiwa hao ni:
1.SILVESTER s/o MUSSA @ KINGWENDU @TAMATI 31yrs mkazi wa Mkuyuni Tambukareli – Mwanza
2.SADIKI s/o HAMISI RUSHIKAMWA @SADICK MILAMBO @WHITE 28yrs mkazi wa Mihogoni –Tabora
3. ABEL S/O BENEDICT @MWENDO WA SAA 23yrs Mfipa mkazi wa Urambo Muungano
4. FRANCIS S/O KASHINJE @MASANJA 38yrs Msukuma, mkazi wa Nansio – Ukerewe
5. HAJI S/O ATHANAS @SIMBA,50yrs Mnyamwezi Mkazi wa Usoke
6. MUSSA S/O KHATIBU ALLY@MUSSA BONGE,49yrs Mnyamwezi Mfanyabiashara wa Nafaka na mkazi wa Mwanza Rd.
7.RAMADHANI S/O KASSIM MKUNYA@RAMA MANYWELE@RAMA MREFU Mkazi wa Tabora
Baada ya mahojiano nao walikiri kushiriki matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo tukio la tarehe 28/04/2014 katika tarafa ya usoke ambalo lilipelekea kuuwawa kwa askari wawili. Baada ya kupekuliwa walipatikana na silaha Pistol Glock17 namba TZ Car 91968 ikiwa na magazine yenye risasi tano.Aidha katika Msako unaoendelea huko Urambo tarehe 25/05/2014 majira 0200hrs alikamatwa mtuhumiwa mmoja na silaha aina ya gobore iliyotengenezwa kienyeji ikiwa imekatwa kitako na risasi 2 za shortgun na 3 za SMG/SAR,upelelezi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUKAMATWA WATUHUMIWA 10 KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI MAGUNIA SITA NA KETE 402:
Katika hatua nyingine msako uliofanyika huko Wilaya ya Kaliua, Nzega na Tabora Manispaa wamekamatwa watuhumiwa wa kumi msukuma wakiwa na gunia 6 za bhangi na kete 402.
1. PINGWA s/o BUHILA, 14yrs, msukuma,mkazi wa mpandamlowoka
2. MAGRETH d/o JULIUS, 15yrs, msukuma mkazi wa mpandamlowoka
3. MALALE s/o KWANGULIJA, 13yrs, msukuma,mkazi wa mpandamlowoka
4. HALIMA d/o MIHAMBO, 70yrs,
5. HASANI s/o HASANI, 40yrs,
6. MRISHO s/o JUMA, 33yrs, M/mwezi, Mtaturu, mkazi wa azimio Isevya,
7. GEORGE s/o BALTAZARI, 31yrs, msukuma
8. BAMKUBWA s/o MOHAMEDI 49yrs mgogo, PAULO s/o BUNDALA, 33yrs, Msukuma
9. JUMA s/o SHIJA, 28yrs, Mnyiramba,
Watuhumiwa watatu ambao wana umri mdogo rbada ya kuhojiwa walikiri kufanya biashara ya uuzaji wa bhangi ambayo hutumwa na wazazi wao aidha watuhumiwa wengine wamekiri kuwa ni wauzaji wa bhangi. Wazazi wa watoto hao wanatafutwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani mara moja.
KUPATIKANA MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE MOSHI: mnamo tarehe 21/05/2014 huko eneo la ng’ambo kata ya Ng’ambo manispaa ya Tabora alikamatwa CHAUSIKU d/o ABDALA, 38yrs, M/mwezi, mkazi wa Ng’ambo akiwa na mitambo 5 ya kutengenezea pombe ya moshi,baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kuwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo. Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.
KUKAMATWA WATUHUMIWA 8 NA LITA 110 ZA POMBE YA MOSHI:
Huko Wilaya ya Igunga na Sikonge 8 na jumla ya lita 110 za pombe ya Moshi,watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na:
1. MWAJUMA d/o SALEHE, 45yrs, mnyaturu, mkazi wa mwanzugi na
2. ALLY s/o MUSA, 24yrs, muha,
3. KATALINA d/o AMOUR,
4. MAERRY d/o LUKAS
5. EMMANUEL s/o KILASA, 29YRS M/MWEZI,
6. CATHERINE D/O MPALASINGE,50yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
7. MARIA D/O DAUDI 24yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
8. KAUMBWE S/O IBRAHIM 26yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo.watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.
AJALI YA MOTO KUSABABISHA KIFO: Mnamo tarehe 21/05/2014 huko kijiji cha Mwanzugi, kata/tarafa na wilaya ya Igunga moto uliwaka kwenye chumba cha kufanyia biashara ya mkaa katika nyumba ya NTEJO s/o ZANZIBAR, 42yrs, Msukuma, mkazi wa Mwanzugi na kusababisha kifo cha DORA d/o BUNDALA, 35yrs, Msukuma, mkazi wa Mwanzugi na majeruhi mmoja ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Igunga. Chanzo cha moto huo marehemu alikuwa anapika katika jiko la mkaa huko ndani ya nyumba kukiwa na madumu yaliyokuwa na petrol na kusababisha mlipuko huo. Mmiliki wa nyumba hiyo alitoweka mara baada ya tukio hilo na kwenda kusikojulikana. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.
KUKAMATWA KWA GARI LINALOSADIKIWA KUWA LA WIZI
Mnamo tarehe 25/05/2014 majira ya saa 1830hrs huko maeneo ya Kanyenye Kata ya Kanyenye Manispaa ya Tabora alikamatwa Moses S/O Meshack 37yrs Muha ,Mkazi wa Ipuli akiwa na gari namba T 636 DUW Toyota Harrier rangi ya Metalic Silver,Chassis No.100078234,Engine No.1MZX 0986347 ambalo alishindwa kulitolea maelezo.Uchunguzi wa awali unaonesha gari hilo mmiliki halali ni Bw.Abrahamu S/O Joseph Myahucho mkazi wa Dar Es Salaam.Upelelezi unaendelea kuhusiana na uhalali wa gari hilo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linazidi kutoa rai kwa wananchi kuzidi kushirikiana nasi katika kupambana na uhalifu na wahalifu kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini uhalifu na kuwakamata.Aidha kufuatia matukio ya moto tunatoa wito kuacha tabia ya kuhifadhi mafuta hasa ya Petrol/|Diesel ndani ya nyumba kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na mali zao.


Imetolewa na :-

Suzan S. Kaganda -ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.

Post a Comment

0 Comments