Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, mpango kwa ajili ya kuachiliwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara nchini Nigeria unakaribia kufikiwa wakati serikali ya Nigeria ikiitisha mpango wa makubaliano.
Baadhi ya wasichana walitarajiwa kuachiwa huru kwa kubadilishana na wafungwa wa Boko Haram.
Kundi la Boko Haram limewateka zaidi ya wasichana 200 waliokuwa shuleni Aprili 14 mwaka huu na kuamsha hisia kali miongoni mwa watu wengi wakiwemo viongozi wakubwa duniani.
Serikali ya Nigeria iko chini ya shinikizo la kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya kukabiliana na kundi la Boko Haram ambalo limewateka wasichana hao.
Maelfu ya watu wamefariki tangu kundi la Boko Haram lilipoanza kampeni ya nguvu dhidi ya serikali ya Nigeria mwaka 2009.
0 Comments