Header Ads Widget

INASIKITISHA NA NI UKATILI: MTOTO MLEMAVU AFUNGIWA NDANI NA MAMA YAKE KWA MIAKA 9 KOROGWE TANGA




Mtoto mwenye ulemavu wa akili wilayani Korogwe, mwenye umri wa miaka 15, amefungiwa chumbani na mama yake wa kambo kwa muda wa miaka 9, ambapo amekuwa akijisaidia humo choo kikubwa na kidogo, kisha kuwekewa chakula katika bakuli lake maalum ndani ya chumba hichoMwandishi wetu ameshuhudia mtoto huyo akiwa chumbani na upande mmoja wa kanga huku kukiwa na vinyesi na bakuli lake analowekewa chakula mithili ya mnyama
.


Mama mlezi wa mtoto huyo mlemavu aliyejulikana kwa jina la Khadija Makame alipoulizwa kuhusu kitendo cha kumfungia ndani mtoto huyo, amesema kuwa huwa anamtoa nje kwa chakula na hata kumsindikiza chooni, majibu ambayo majirani walipingana naye baada ya kushuhudia ndani ya chumba chake kukiwa na vinyesi na bakuli lake la kulia

Post a Comment

0 Comments