Header Ads Widget

INASEMEKANA KUWA JOH MAKINI NA NIKKI WA PILI NDIO WAMEAU KUNDI LA NAKO 2 NAKO NA RIVER CAMP! KAMA HUJUI BASI SOMA HAPA






Mara nyingi Nikki wa Pili kama msemaji wa kundi la WEUSI amekuwa akinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai kwamba weusi si kundi bali ni kampuni ambayo haina uhusiano wowote na kundi la rivercamp soldiers ambalo lilikuwa linaundwa na Joh Makin, Nikki wa Pili, Bonta na wengineo na pia haliingiliani na kundi la Nako2Nako lilikuwa likiundwa na Gnako&Lord eyez na waliojitoa mapema Bu Nako na Ibra da.

Nikki anasema kuwa kuwa makundi ya rivercamp soldier na Nako2Nako hayajafa na bado yanaendelea na shughuli zao, ukweli ni kwamba makundi haya wawili yalishakufa tangu tu pale kundi la weusi lilipoundwa. Toka kundi la weusi limeundwa lini tumesikia kazi ya nako2nako? lini tumesikia kazi ya rivercamp soldier kundi ambalo lilikuwa lipolipo tu halina mbele wala nyuma.

Joh makini na Nikki wa Pili ndio wameyaua haya makundi kwasababu za kimaslahi, kwanini Bonta hayupo kwenye kundi la WEUSI? Walitumia vigezo gani kuunda hiyo kampuni?

Kama wao walihisi wakifanya nyimbo kati ya John Makini, Nikki, G nako na Lord Eyez ndio inakuwa nzuri basi ni vema wakawa wawazi kuwa washajitoa kwenye makkundi yao na waunda kundi jipya kuliko kuwadanganya wenzao na watanzania kwa ujumla.

Kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuunda hiyo kampuni ya weusi wakati kundi lenu tu la rivercamp soldiers halijafanya chochote kinachoonekana kwa jamii? Kulikuwa na umuhimu gani wa kuunda kampuni ya weusi wakati kundi la nako2nako lilikuwa bado halijasimama vizuri? ni kipi hasa mlichokuwa mkikitafuta ambacho hakipo kwenye makundi yenu?

MCHAWI WA MSANII, NI MSANII MWENYEWE. OVER

Post a Comment

0 Comments