
Klabu ya Yanga, imetangaza kuachana na kocha wake, Nasreddin Nabi baada ya kumalizika kwa mkataba wake. Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikutana na Nabi na kuzungumza naye kuhusu kusaini mkataba mpya lakini Nabi ameomba kupewa nafasi ya kwenda kutafuta changamoto mpya.

0 Comments