Mwanaume Mmoja apoteza kazi kwa Kudaiwa kutumia muda mrefu chooni wakati wa kazi
Mchina mmoja alifukuzwa kazi na kampuni yake kwa kutumia muda wa mapumziko yake chooni muda mrefu ambayo yalichukua hadi saa sita kwa siku kadhaa kama ilivyoripotiwa na South China Morning Post.Mfanyakazi huyo, aliyetambuliwa kama Bw Wang, alikuwa ametafuta hatua za kisheria dhidi ya mwajiri wake na kudai kufukuzwa kazi isivyofaa.
Hata hivyo, hata mahakama za China zilitoa uamuzi kwa upande wa waajiri, na kukataa kukubali rufaa ya Wang.
Kulingana na ripoti ya SCMP, Wang alijiunga na kampuni hiyo mnamo Aprili 2006 na alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa kawaida hadi 2014.
Shida za Wang zilianza mnamo Desemba 2014, alipopata matibabu ya ‘tatizo la anorectal’, ambalo lilikuwa sababu ya choo chake cha mara kwa mara.
0 Comments