
Baada ya kufuzu kucheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa Yanga SC sasa watacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya USM Alger ya Algeria dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast.

Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa nyumbani na ugenini na Yanga ataanza kucheza nyumbani Mei 28 2023 na marudiano ni June 3 2023.
Game ya nusu fainali ya pili itachezwa saa 22:00 leo nchini Algeria kati ya USM Alger dhidi ya Asec Mimosa baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kule nchini Ivory Coast kumalizika 0-0.







0 Comments