Baada ya Club ya Yanga kutangaza kwa mara ya kwanza kiingilio cha juu zaidi katika mchezo wa soka Tanzania inayohusisha club hiyo leo wametangaza kuisha kwa tiketi hizo.
Yanga ambao wanatarajia
kucheza fainali yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika siku ya Jumapili ya Mei 28 2023 dhidi ya USM Alger katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jana walitangaza tiketi za VIP A kuwa ziuzwe Tsh 100,000/= (laki moja) badala ya Tsh 30,000 kama ilivyozoeleka leo Yanga wametangaza kuwa tiketi za VIP A zote zimeisha ikiwa ni siku 5 kabla ya mchezo.
Kwa sasa tiketi zilizosalia ni VIP B Tsh 30,000/=, VIP C Tsh 15,000/= na mzunguuko Tsh 5000, hii ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na marudiano itakuwa June 3 2023 nchini Algeria, mchezo huo Yanga wameupa kaulimbiu ya “WHY NOT US” wakiwa na maana “
KWA NINI SIO SISI”
0 Comments