Header Ads Widget

Rais Samia Aunda Kamati Ya Kutathmini Utendaji Kazi Wa Wizara Ya Mambo Ya Nje



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Ili kutekeleza azma hiyo Dkt Samia amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, Rais Samia amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:

1) Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

2) Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

3) Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

4) Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

Post a Comment

0 Comments