Ndege tatu zikiwa na Watalii zaidi ya 250 zimetua katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA ambapo ndege mbili kutoka Marekani na Isarael zikiwa zimekodiwa na wageni hao kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Nchini Tanzania.
Christine Mwakatobe Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya KADCO inayoendesha uwanja wa ndege wa KIA amesema ujio wa ndege hizo ni kwa mara ya kwanza ikilinganishwa na mwaka jana na hii ni baada ya filamu ya Royal Tour aliyoifanya Rais wa Tanzania Dkt Samia Hassan ya kutangaza utalii.
0 Comments