Header Ads Widget

Shirika La Ndege Nchini (ATCL) Lapata Hasara Ya Bilioni 35.2, Reli 31.2 – Video



KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL), imepata hasara ya Sh bilioni 35.23 katika mwaka wa fedha 2021/22. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza.

Akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2022, CAG Charles Kichere amesema katika ripoti yake imeonesha mwaka wa fedha 2020/21, ATCL ilipata hasara ya Sh bilioni 36.18.

Amesema ripoti yake imebaini katika ATCL walijiwekea lengo la ndege zinazochelewa iwe ni asilimia 8 lakini kupitia ukaguzi wake umebaini ndege hizo kuchelewa kwa kwa asilimia 25.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Sh bilioni 22.8 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 31.2. Kampuni ya Mkulazi ilipata hasara ya Sh bilioni 5.8 mwaka 2020/21 na mwaka uliofuata ilipata hasara ya Sh bilioni 14.3.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilipata hasara ya Sh bilioni 26.3 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 11.9.

Post a Comment

0 Comments