Header Ads Widget

Nuh Mziwanda kuja na studio yake





Baada ya kuachana na Shilole, Nuh Mziwanda anajipanga kufungua studio yake ambayo anadai atafanya kazi na wasanii wakubwa Bongo.


Akiongea kwenye kipindi cha 5 Select cha EATV, Nuh alisema vifaa vyote vipo tayari na bado tu sehemu ambayo studio zake zitakuwepo.



“Nina studio yangu ambayo ipo na tayari na vifaa vyote vipo, bado vitu vidogo ianze kazi. Studio itakuwa inaitwa ‘Last Born Records’ na kwa kuanza nitaanza kufanya kazi na Alikiba huyo ndiye ninayeweza kumuongela kwa sasa ambaye tumeshafanya maongezi,” alisema.


Hivi karibuni Nuh Mziwanda aliachia kazi aliyomshirikisha Alikiba, ‘Jike Shupa.’

Post a Comment

0 Comments