Baada ya michezo mitatu ya Kombe la FA kuchezwa na kushuhudia timu za Dar es Salaam Young Africans, Mwadui FC na Azam FC kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, April 11 2016 ilikuwa zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga.
Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Coastal Union kutokana na timu hiyo kuaminika kuwa chini ya kiwango na Simba kuutawala mchezo, wamekubali kipigo cha goli 2-1 wakiwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 20 na Youssouf Sabo aliyefunga kwa mpira wa faulo. Simba walifanya mabadiliko na kumuingiza Hamis Kiiza ambaye alifunga goli la kusawazisha dakika ya 50 na kuufanya mchezo kuwa sare hadi dakika ya 85 Youssouf Sabo akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyotokana na makosa na Novat Lufungo kumchezea faulo Shiboli.
0 Comments