Header Ads Widget

TEMEKE HAWANA UHAKIKA NA KIPINDUPINDU…!!



DAR ES SALAAM
Siku moja baada ya waziri wa afya kuitaja manispaa ya Temeke kuwa moja ya manispaa zilizo na wagonjwa wa kipindupindu manispaa hiyo imekanusha na kusema kuwa wagonjwa walioko bado hawajathibitika kama wanaugonjwa huo huku wagonjwa wawili kati ya watatu waliokuwa wakisadikiwa kuwa na ugonjwa huo wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Tekeme Bi Sophia Mjema baada ya kutembelea kambi hiyo wagonjwa wanaosadikiwa kuwa na vimelea vya kipindupindu ambapo maafisa wa kambi hiyo wamemhakikishai kuwa bado hakuna mgonjwa aliyethibitika mpaka sasa.
Zaidi ya nyumba 100 na vyoo 100 zimewekewa dawa pamoja na dawa za maji huku taarifa zikisema tangu kuanza kwa ugonjwa huo zaidi ya kaya 24100 zimekwisha kupuliziwa dawa huku wagonjwa waliosadikika kuwa na ugonjwa tangu mlipuko huo uanze wakiwa 817 huku 16 pekee kati yao wakitajwa kupoteza maisha.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewahakikisha zaidi ya wakazi mianne wa mtaa wa Gorota katika kata ya Tuangoma ndani ya manispaa hiyo kuwa manispaa hiyo itahakikisha inatatua kero ya mfereji ambao umekuwa ukitililisha maji katika makazi yao na kuhatarisha nyumba zao.
Awali wakizungumza wakazi hao wamemtaka mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anashughulikia tatizo hilo kikamilifu kwani wao na watoto wao wako hatarini zaidi hasa mvua zinaponyesha.
Ujenzi usiofuata vigezo vya mipango miji umetajwa kama moja ya changamoto ambayo bado inaikabili manispaa hiyo ambapo wananchi wengi wamekuwa wakijenga kiholela na wakati mwingine kusababisha kuziba njia za maji na barabara jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa manispaa.

Post a Comment

0 Comments