Stori za kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea yaUingereza Jose Mourinho kujiunga na klabu yaManchester United zinazidi kushika kasi, licha ya kuwa ni tetesi hadi sasa kuhusu Jose Mourinho kurithi nafasi yaLouis van Gaal ndani ya Man United, stori hiyo inapata nguvu baada ya stori nyingi mwishoni mwa mwaka 2015 zilizoanza kuandikwa kama tetesi zote zilitimia.
Zilianza stori za Raphael Benitez kuwa atafukuzwa Real Madrid kweli stori hiyo ikawa kweli, Jose Morinhokufukuzwa Chelsea ikawa kweli, Pep Guardiola kuwa kocha wa Man City, kweli Man City wamethibitisha, stori mpya kutoka Marca gazeti ambalo stori zake zinaaminika, limetaja tarehe rasmi ya Jose Mourinho kutua Man United.
Marca wameandika kuwa Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa Man United kuanzia July 1 2016, licha ya kuwaMarca wanaripotiwa kuandika stori hiyo kama tetesi, lakini inapata nguvu kutokana na stori nyingi zilizoandikwa kama tetesi msimu huu zimekuwa kweli.
Gazeti la Marca linataja kuwa kama Louis van Gaalakiendelea kufanya vibaya kabla ya msimu huu kumalizika atafukuzwa na nafasi yake kurithiwa kwa muda na Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi na July 1 Jose Mourinhondio anatajwa kuwa atakuwa kocha rasmi wa Man United.
0 Comments