Header Ads Widget

Serena Williams kwenye hatua nyingine ya ushindi dhidi ya Maria Sharapova..


Nyota wa tennis duniani Serena Williams ameendelea kuonyesha kwamba yeye ndio bora zaidi baada ya kumshinda mpinzani wake Maria Sharapova kwenye michuano ya wazi ya Australia Open.

Huu ni ushindi wa kumi na nane mfululizo kwa Serena Williams dhidi ya Sharapova, na kwa ushindi huo Serena anasonga mbele kuingia hatua ya nusu fainali.

Bingwa huyu mtetezi wa taji hilo alipata ushindi wa seti 6-4 6-1 katika mchezo ulifanyika kwenye uwanja wa Melbourne Park.

Serena atachuana na Agnieszka Radwanska katika hatua ya nne bora.
 

Post a Comment

0 Comments