Header Ads Widget

Kilichonifikia kuhusu tukio la kuzuka moto Wizara ya Mambo ya ndani Dar leo.. (Pichaz)




Huenda umekutana na stori mitandaoni au picha kuhusu tukio la ajali ya moto katika jengo la Wizara ya Mambo ya ndani, posta Dar es Salaam.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Advera Senzo Bulimba amesema ni kweli kulitokea cheche za moto katika jengo hilo katika ghorofa ya nne, taarifa zikatolewa kwa vikosi vya zimamoto ambao walifika na kugundua kuwa chanzo cha moto huo ilikuwa kwenye cyling board.

Hakuna mfanyakazi yoyote katika jengo hilo aliyedhurika kutokana na tukio hilo na kikosi cha zimamoto waliweka kuuzima kila kitu kikawa sawa.


Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Advera Senzo Bulimba


Baadhi ya wafanyakazi wakiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo.


Baadhi ya askari wakitoka nje ya jengo hilo baada ya kutokea tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments