Header Ads Widget

Serikali mkoani Kagera imeteketeza kwa moto zana haramu za uvuvi.





Serikali mkoani Kagera imefanikiwa kuteketeza kwa moto zana haramu za uvuvi zenye thamani ya zaidi ya shiringi milioni mia sita ambazo zilikuwa zikutumika kufanyia uvuvi haramu katika ziwa Victoria.
Akiongea mjini Bukoba afisa mfawidhi wa uvuvi mkoani Kagera Apolinary Kyojo amaesema uvuvi haramu katika ziwa Victoria bado nitishio kubwa kwakuwa wavuvi waliowengi hutumia zana haramu ambazo maranyingi zimekuwa zikiteketeza samaki wachanga na kuhalibu mazalia ya samiki hali ambayo inaweza kupelekea kutoweka wa samaki katika ziwa hilo.

Akizungumza mara baada ya kutekeza zana hizo haramu za uvuvi mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella amesema serikali haikotayari kuwavumilia wavuvi wanaokiuka sheria na kanuni za uvuvi kwa kutumiwa zana haramu pamoja na madawa yenyesumu kali ambayo yamekuwa yakiathiri mazalia ya samaki huku akiahidi kudhibiti vyanzo vya zana haramu ambazo maranyingi zimekuwa kikwazo katika uvuvi wa samaki.

Nao baadhi ya maofisa wa doria katika ziwa Victoria wamesema pamoja kukamata zana hizo haramu pia wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika opresheni zao ikiwemo wavuvi kubuni mbinu mpya ya kuficha zana za uvuvi kwa kuzichimbia chini ya mchanga huku baadhi ya wananchi wakilalalamikia kupanda kwa bei samaki kiholela kunakosabishwa na tatizo la uvuvi haramu.
chanzo: ITV

Post a Comment

0 Comments