Klabu ya Manchester United ambayo bado inahusishwa kuwa katika kipindi kigumu cha mpito, kwani toka aondoke aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson kunaonekana kutokuwa na matokeo mazuri kwa timu hiyo licha ya kuwa Louis van Gaal ni kocha wa pili kuifundisha Man United toka Sir Alex Ferguson aondoke. Usiku wa December 8 Man United iliaga rasmi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 kutoka Wolfsburg. Hivyo kuna stori kutoka sokkaa.com kuwa, huenda Van Gaal akaondoka na nafasi yake kurithiwa na mmoja kati ya makocha hawa.
5- Ryan Giggs ni kocha msaidizi wa klabu ya Man United hata wakati anafukuzwa David Moyes yeye ndio alirithi nafasi ya ukocha mkuu na alipokuja Louis van Gaal akaendelea kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo. Ryan Giggs anatajwa kuwa na nafasi ya kumrithi Van Gaal kutokana na mashabiki kuwa na imani nae ila yeye ni moja kati ya watu wasiounga mkono mfumo wa Van Gaal.
Ryan Giggs
4- Jose Mourinho ni moja kati ya makocha waliofanikiwa katika historia ya soka, huyu alikuwa ni moja kati ya makocha waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kumrithi Sir Alex Ferguson, kabla ya David Moyes kushika nafasi hiyo, licha ya kuwa ana wakati mgumu kwa sasa na klabu yake ya Chelsea, Mourinho ameshinda mataji mawili ya UEFA akiwa na klabu mbili tofauti sambamba na kutwaa mataji ya Ligi mbalimbali duniani. Huyu nafasi yake inatajwa kuwa kubwa kumrithi Van Gaal.
Jose Mourinho
3- Carlo Ancelotti aliwahi kuvinoa vilabu vya Chelsea, Real Madrid na sasa yupo nje ya uwanja kwa kuwa hana klabu ya kuifundisha ila siku kadhaa nyuma, yeye alikiri hadharani kuwa anatamani kupata nafasi ya kuifundisha Man United, baada ya kuulizwa swali na waandishi ila alikiri kuwa yupo radhi kusubiri hadi mwaka 2017 ambapo Louis van Gaal atakuwa anamaliza mkataba wake, ila huenda asimalize na akafukuzwa kama mambo hayataendelea kuwa mazuri.
Carlo Ancelotti
2- Diego Simeone ni kocha wa klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, stori ambazo zinaripotiwa kutoka wiki kadhaa nyuma ni kuwa Diego Simeone ameomba uongozi wa Atletico Madrid kuwa, katika mkataba wake kiwekwe kifungu kinachomruhusu muda wowote kuvunja mkataba wake. stori zinaeleza kuwa Simeone huu ndio utakuwa msimu wake wa mwisho kuifundisha Atletico Madrid, hivyo stori zinatajwa kuwa Man United wanavutiwa na kocha huyo ambaye mwaka 2013 alishinda taji la Laliga na kuifikisha fainali ya UEFA Atletico Madrid.
Diego Simeone
1- Pep Guardiola anatajwa kukataa kuongeza mkataba wenye thamani kubwa wa kuendelea kuifundisha FC Bayern Munich, licha ya kuhusishwa kwa karibu kutaka kujiunga na Man City, Pep Guardiola anaripotiwa kuwa yupo tayari kusubiri hadi mwaka 2017, ili arithi nafasi ya Louis van Gaal ambaye mkataba wake utakuwa unamalizika.
Pep Guardiola
0 Comments