Bado Tanzania iko kwenye Majonzi siku moja baada ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Haule Filikunjombe, Rubani Captein William Silaa, na watu wengine wawili, Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule.
Taarifa nyingine imeandikwa kuhusu Helicopter ambayo Marehemu hao wanne wamepata nayo ajali katika Mbuga ya Selous, kwenye Stori hiyo ametajwa Mwanasiasa mkubwa Kenya ambaye pia ni mmoja ya Viongozi wa Muungano wa Vyama vya CORD, Kalonzo Musyoka kwamba ndiye mmiliki wa Helicopter hiyo ambaye aliikodisha TZ katika msimu huu wa Kampeni.
Helicopter hiyo aina ya Eurocopter AS 350B3 Écureuil ilinunuliwa na Mwanasiasa huyo mwaka 2013 wakati wa shughuli za Uchaguzi Mkuu Kenya na baada ya hapo alikuwa akiikodisha kwa watu mbalimbali mpaka October 15 2015 ambapo ilipata ajali na kuteketea kwa moto katika Mbuga ya Selous na kusababisha Vifo vya watu hao wanne.
0 Comments