Header Ads Widget

HABARI MPYA: AJIRA MPYA ZA WALIMU KWA MWAKA 2015 ZIMETOKA... BOFYA HAPA KUONA MAJINA

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YANGU!..

A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-

i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;

ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari

iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari


B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;

ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;

iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;

iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na

v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.

Bonyeza Hapo Chini Kuona Orodha Ya Majina:


1.Ajira za Walimu wa Cheti (Shule za Msingi) 2015.-<>

2.Ajira za Walimu wa Sayansi wa Shahada na Stashahada kwa Mwaka 2015.--<>

3.Ajira za Walimu wa Masomo ya Sanaa na Biashara Ngazi ya Shahada na Stashahada--<>

Post a Comment

0 Comments