Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Uganda Kansiime Jemimah maarufu kama -Panadol wa Basajja- amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka ya kusambaza picha za uchi kinyume na sheria za nchi.
'Panadol wa wanaume' ambalo ni jina la kisanii la mwimbaji chipukizi wa Uganda-Kansiime Jemimah amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka hayo.
Msanii huyo wa kike alikamatwa pamoja na mtengezaji wa muziki wake mwezi uliopita kwa kile waziri wa maadili anasema ni kuhusiana na picha za uchi.
Panadol ametoa vibao kadhaa katika mahadhi ya kufoka lakini ule ambao umemletea shida unaitwa Ensolo Yange yaani mnyama wangu.
Katika video ya wimbo huo kuna sehemu ambapo yeye mwimbaji akiwa kama mhusika mkuu anaonekana akivaa chupi ya G-string huku makalio yake yakiwa nje.
Na pia kuonyesha mapaja yake na baadhi ya maneno ya muziki wake yakiwa
Kwa baadhi wanatafsiri maneno na picha hizo vingine na serikali kusem ani kinyume na sheria.
Mwaka jana sheria mpya dhidi ya picha chafu ilipitishwa ambapo ni marufuku kuuza au kupatikana na picha za uchi. Adhabu ya mtu anaepatikana na hatia ni faini ya shilingi za Uganda laki mbili sawa na dola nane au kifungo cha miaka mine au vyote viwili.
Video hiyo ya utatanishi ilitayarishwa na kijana Muchwa Mugisha maarufu kama Didi ambae yeye alikiri kosa hilo 28 Oktoba na kuwekwa ndani na bada kulipa faini, lakini Panadol akakanusha madai hayo na ndio leo ameletwa mahakamani lakini pia kwa mara nyingine amekanusha madai hayo na hiyo kurejeshwa rumande hadi Disemba 2 mwaka huu.
Sheria hii ya picha za ngono mwanzo ilizusha mgogoro kwani ilipewa jina la sketi fupi na baada ya watu kulalamika kipengee cha sketi fupi kikatolewa.
0 Comments