Header Ads Widget

ROONEY AKABIDHIWA KITAMBAA CHA UNAHODHA ENGLAND



Wayne Rooney akikabidhiwa kitambaa cha Unahodha wa England mazoezini wiki hii

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amekabidhiwa rasmi kitambaa cha Unahodha wa timu ya taifa England na kocha Roy Hodgson jana kuahiria zama mpya Three Lions.
Kocha wa England, Hodgson alitangaza wiki iliyopita kwamba Rooney atakuwa Nahodha wake mpya kufuatia kiungo Steven Gerrard kustaafu soka ya kimataifa.



KIKOSI CHA ENGLAND KITAKACHOCHEZA NA NORWAY

Hart; Stones, Jones, Cahill, Baines; Henderson, Wilshere; Oxlade-Chamberlain, Rooney, Sterling; Sturridge.
Rooney - ambaye pia aliteuliwa kuwa Nahodha wa klabu yake Manchester United msimu huu- sasa ataiongoza England kwa mara ya kwanza usiku wa leo katika mchezo wa kirafiki.
England inatarajiwa kumenyana na Norway katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Wembley kabla ya kusafiri hadi Uswisi Jumatatu kwa ajili ya mchezo wao wa ufunguzi wa kufuzu michuano ya Ulaya.
Rooney, ambaye sasa ana umri wa miaka 28, ameichezea mechi 95 England tangu aichezee kwa mara ya kwanza mwaka 2003.
na BIN ZUBERY

Post a Comment

0 Comments