Header Ads Widget

MSANII LADY JAY DEE AUNGANA NA MARIE STOPES TANZANIA KATIKA KAMPENI YA UZAZI WA MPANGO


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia) akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady jaydee' katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es Salaam jana.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady Jaydee', ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Marie Stopes,katika kampeni za uzazi wa mpango.
Akitangazwa rasmi kuwa balozi mpya msanii Jay Dee aliibua shangwe na nderemo zilizotoka kwa baadhi ya wazazi na watu waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za MST zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Jay Dee sasa anaungana na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua Maisha” ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa rasmi, Jaydee alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo ambayo anaamini ataitendea haki kulingana na nafasi yake kwa jamii.
“Nina furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu wanafanya mengi kuwawezesha kina mama kusimama na kujitegemea, na pia naamini nitafanya kazi nzuri kwa ushirikiano na Marie stopes ili kuiwezesha Jamii kufikia na kuelewa vyema lengo la Uzazi wa mpango''. alisema Jay dee
Lengo kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza: “siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa kuacha masomo kutoka na ujauzito. Mimi nimeamua kusaidiana na Marie Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa kutumia uzazi wa mpango”.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana, 54% wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa kubadili na kukuza hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo iwapo watapata msaada.
Akiwa amesimama Pamoja na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema: “Leo hii nchini Tanzania, mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri wa miaka 19 wamekwisha kuwa wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wamo katika ndoa za kulazimishwa.
Zaidi ya hayo, kama binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule na huo ndio unakuwa mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri ambayo vijana wetu wanahitaji iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa taifa letu na kuliweka kuwa katika kipato cha kati (middle income). Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua kwa taifa letu, hivyo ni jukumu letu kuwapa fursa hizo”.
“Nina imani kubwa kuwa tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila mmoja atambue kuwa ana haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto, na pia idadi ya watoto wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine zinaweza kukusaidia kumaliza masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi hii kwenya Nyama Choma Festival, Dar es Salaam!”
Tukio hili la Lady Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam litaonyeshwa jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV. Kituo hiki kilichopo Mwenge ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa huduma za uzazi wa mpango kwa Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.

Post a Comment

0 Comments