Header Ads Widget

Hii ndiyo List ya viwanja 7 vya ndege vilivyo busy duniani! Afrika je?

Wakati nchi kama Tanzania inapambana kujenga viwanja vya ndege ili ndege kubwa kama za Fastjet ziweze kutua sehemu kama Musoma, Kigoma na Arusha baada ya kuweza kufanya safari zake kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Dar na Mwanza, ifuatayo ni list ya viwanja vya ndege duniani ambayo hutoka kila mwaka.

Kiwanja kilichoshika namba moja kwa kuwa busy kuliko vyote duniani ni kiwanja cha Atlanta Georgia Marekani wanakotoka mastaa kama rapper T.I ambacho kwa mwaka 2013 pekee kimehudumia abiria milioni 94.4, namba mbili inashikwa na Beijing Capital International Airport ambacho kilihudumia abiria milioni 83.7

Kiwanja namba 3 ni cha London Heathrow Airport kilichobakia kwenye nafasi hiihii ya mwaka jana ambapo kimehudumia abiria milioni 72.4 huku kiwanja cha Tokyo Japan (Haneda) kikishika namba 4, cha tano ni Chicago O’Hare International Airport nchini Marekani na cha sita ni Los Angeles International Airport hukohuko Marekani.

Kiwanja cha ndege Dubai kimeshika namba 7 kutoka namba 10 mwaka uliopita ambapo kimehudumia abiria milioni 66.4 ambapo kiwanja cha ndege cha Paris kimeshuka nafasi moja kutoka ya 7 mwaka uliopita na kushika ya nane mwaka huu, ya tisa imeshikwa na kiwanja cha ndege cha Dallas/Fort na namba 10 imeshikwa na kiwanja cha Jakarta Indonesia.  
credt: millardayo.com

Post a Comment

0 Comments