Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Lukumai kulia akiwekeana saini ya Mkataba na Mama Fatuma Karume.
BENKI ya CRDB imesema ndani ya miaka mitano Yanga SC inaweza kuikaribia kiuchumi Manchester United ya England, iwapo wanachama wake watatumia vizuri fursa ya kuichangia klabu yao kupitia benki hiyo.
Yanga SC imeingia Mkataba huru wa kuanzia na benki ya CRDB kwa ajili ya kuchapisha kadi mpya za wanachama wake, zitakazojulikana kama Gold Card baada ya kuachana na beki ya Posta.
Mkurugenzi Mtendaji wa DRCB, Dk Charles Kimei ametiliana saini Mkataba huo na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Mama Fatuma Karume leo katika ofisi za benki hiyo, Mtaa wa Azikiwe, Dar es Salaam.
Kimei amesema kwamba kadi hizo zitapatikana kwa gharama ya Sh. 8,000 lakini kwa wateja wapya ambao ni wanachama wa Yanga SC watapatiwa bure.
Amesema malengo waliyojiwekea CRDB ni kukusanya wanachama 100,000 ndani ya mezi ya miwili kwa kuanzia. Amesema wanachama wa Yanga SC wanaweza kuichangia klabu hiyo kiasi chochote cha fedha kwa matakwa yao kulingana na uwezo wao.
“Endapo wanachama wa Yanga watachangamkia kadi hizi na kulipa michango yao, Yanga inaweza kuwa na nguvu ya kiuchumi kiasi hata cha kuikaribia Manchester United ndani ya miaka mitano tu,”amesema Kimei.
Amesema anaamini Yanga SC ni klabu kubwa na ina wanachama wengi na kwamba hata baadhi ya wateja wake ni wanachama wa klabu hiyo. Amesema huduma hiyo inapatikana nchi nzima katika matawi yote ya benki ya CRDB.
Kwa upande wake, Mama Karume, mke wa rais wa zamani wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume (sasa marehemu) ameishukuru CRDB kwa kuisaidia Yanga SC katika hilo na akawapongeza viongozi kwa juhudi zao za kuipata benki hiyo.
Juni mwaka huu, Yanga SC iliingia Mkataba wa aina hiyo na benki ya Posta, lakini imeamua kuachana nayo kwa madai malengo hayajatimia.
0 Comments