
Masanja ambaye pia ni mchungaji amefunguka na kueleza kila kitu kuhusiana na ishu hiyo huku akikanusha vikali kuwepo kwa uvunjifu wa kundi hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu, Masanja alisema kuwa kundi hilo halijavunjika kama ilivyoripotiwa na kudai kuwa litarejea kama kawaida kuanzia mwezi Septemba mwaka huu na kuendelea kubamba kama ilivyozoeleka kipindi cha nyuma na kufanikiwa kujizolea umaarufu wa kutosha nchini.
“Kikubwa tu watu waachane na hizo tetesi Ze Komedi kwamba imevunjika, nasema kwamba haijavunjika wala hatujasambaratika hata kidogo, tupo na tutaendelea kuwepo. Rasmi tutaanza kazi Septemba mwaka huu,” alisema Masanja.
0 Comments