MWANADADA anayefanya vizuri katika filamu, Lucy Komba, amesema harusi yake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni itakuwa ya kawaida sana ‘simple’ kuliko harusi nyingine za wasanii ambazo zimewahi kufanyika.
Akizungumza na safu hii, Komba alisema anafanya hivyo kutokana na mume anayemuoa kutotaka makuu, ambapo watu 300 wanatarajia kuhudhuria.
Kuhusu mipango ya harusi, alisema inaenda vizuri na tayari zaidi ya nusu ya aliowapa mwaliko wamethibitisha kuhudhuria.
Sherehe za harusi hiyo zitafanyikia ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
0 Comments