Header Ads Widget

DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZA BAADA YA TUZO 'PASSPORT YANGU IMEJAA KWA SAFARI ZA NJE NA BADO NINA VISA KIBAO MKONONI'









AZUNGUMZIA KUFANYA VIDEO NJE YA NCHI:

''Unajua madongo mengi yanayorushwa kuhusu wasanii wa bongo kufanyia video nje najua narushiwa mimi ila naamua kukaa kimya tu''...........




Anaendelea..." Mie siwezi kufanya video na madirector wa kibongo kwa sasa kwa sababu ni wazinguaji sana....Tatizo sio quality inayonikimbiza bongo ila utendaji wa kazi haswa ndio tatizo kubwa,,,,hawathamini wateja wao(directors).

Mtu unamlipa pesa ila kufanya kazi inabidi umbembeleze,Nimeshawahi kususa video mbili kwa director nikiwa nimeshazilipia kila kitu, baada ya kuzifatilia nakuishia kuzungushwa miezi minne. Ni video ya 'Nimpende nani na Lala salama', Nimeshawahi kumlipia ticket ya ndege director twende tukashoot South Africa na akaishia kunizingua.

Mtu unaamshwa na director saa kumi na mbili asubuhi ufike location,unafika unamsubiria yeye anatokea saa 4.




MaDirector wa nje wanakutreat mpaka unaona thamani yako kama msanii, pia wanaangaikia mpaka kukuconnect na media kubwa. Hapa kwetu ukisharecord unaangaika mwenyewe na bado mtu anakutreat kama anakupa msaada wakati pesa yote aliyotaka umempa''.




Azungumzia Changamoto:




''Changamoto kubwa ni kupata lawama,ujue kwa sasa nina marafiki wengi na najuana na watu wengi sasa kumridhisha kila mtu inafika kipindi nashindwa...........unakuta unapata maombi mengi mfano ya interview mfano, sasa ratiba yangu ni tai sana ata muda wa kupumzika nakosa na ninatakiwa uku na uku, nikikosa uku unakuta mtu anajisikia vibaya anaona umeanza kumdharau na ata nafasi ya kumwelewesha nashindwa Dah hicho kitu uwa kinaniumiza sanakuliko vyote sababu mie sipendi kumuudhi mtu anayenisapot ila kama binadamu sometimes nashindwa you know msayn! ''.




'' Changamoto nyingineyo, nina watu wanaonpenda na kuniamini sana na wanaamini sitowaangusha ata siku moja. So wanafanya nifanye kazi kwa nguvu nyingi nisiwaangushe''........Anaende lea.'' unakuta mtu ni shabiki wako mnakutana airport,umechoka kinoma unawaza kupumzika tu, anatokea anaomba mpige picha, inabidi ukubali na utupie na tabasamu japo upo hoi''




Aulizwa na Vanessa kama ana uwezo wa kurap, anaomba apewe beat achane....apewa beat ya laini aikataa anaomba beat ngumu........Anaonyesha uwezo wa kurap pia.







MENGINE ALIYOONGEA.....

'' Unajua muziki wako kwa sasa ukipita Nigeria ndio umepita Africa''.




'' Passport yangu ya pili inakaribia kuisha hapa nilipo nina visa kibao mkononi...unajua nasafiri sana ninachoka lakini siwezi kukaa chini inabidi nitumie huu wakati''




'' Wategemee collabo ya nyingi sana, zingine ni za nje ya Africa....nikitoka hapa naenda studiio kurekodi nyimbo ya collabo na Case wa Nigeria ni nyimbo yake''




'' Idea ya video ya Mdogomdogo ilianzia kwa Adam Kuambiana, baadae tukaiboresha mimi na Wema''




'' Nimemuona Rihana LIVE,alikaa nyuma yangu siku iyo.....yani nilikuwa sielewi chochote kugeuka nyuma namuona mtu kama Rihana,sikuamini ikabidi nigeuka zaidi ya mara mbili uku najiuliza hivi uyu si Rihana uyu?? ikabidi nipotezee kama sijashtuka vile,ila kwa kweli kushangaa sio siri hakuniishi sababu vitu vingi tulikuwa tunavisikia tu nakuviona vya ajabu''




NB; Lugha alizotumia ni Kiswahili na Kiingereza cha kuulizia njia.







Asanteni!!!!!!!!

Post a Comment

0 Comments