LUIZ Felipe Scolari amesema hatajiuzulu katika nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Brazil, licha ya timu yake kufungwa mara ya pili mfululizo ndani ya siku tano.
Brazil walifungwa mabao 7-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Belo Horizonte siku ya jumanne ya wiki hii na usiku wa jana walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi na kumaliza katika nafasi ya nne ya fainali za 2014 za kombe la dunia kwenye ardhi yake.
Kabla ya mashindano haya, Brazil ilikuwa haijapoteza mechi nyingi za nyumbanii tangu mwaka 2002 na walikuwa hawajawahi kufungwa nyumbani katika mashindo ya mpira wa miguu tangu mwaka 1975, lakini kufungwa mara mbili mfululizo ndani ya siku tano kumewachangaya mashabiki na waandishi wa habari wan chi hiyo.
Lakini Scorali alikutana na waandishi wa habari baada ya kufungwa na Uholanzi na kusisitiza kuwa shirikisho la soka nchini Mbrazil litaamua hatima yake ya baadaye.
“Ulikuwa mchezo wenye nguvu sawa,” alisema. “Wachezaji wanatakiwa kupongezwa kwa jinsi walivyocheza. Hatukucheza vibaya-hayo ndio maoni yangu”.
“Kwasasa sio muda muafaka wa kuzungumzia hilo, “ alisema Scolari. “Nitaandika ripoti yangu na kumwambia rais wa CBF ni kitu gani nadhani hakikwenda sawa, yeye ataamua nini anataka kwa baadaye. Tumepoteza mechi nyingine, lakini maisha yanaendele”.
“Mwaka mmoja uliopita nilishinda kombe la mabara,” aliongeza. “Makosa hayako kwa makocha. Kitu ni kwamba tuna timu ya vijana sana. Hatujazalisha wachezaji wa kutosha, kwahiyo sio kazi rahisi hata kama Kocha mwinine atakuja”.
0 Comments