Header Ads Widget

MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AUAWA NA POLISI MKOANI MBEYA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI



Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akionyesha silaha aina ya Ak 47 kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake










Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limeua Mtuhumiwa wa ujambazi Joseph Kapinga Mkazi wa Mafiga Mkoani Morogoro akiwa na silaha aina ya Ak 47 yenye risasi 25 kwenye magazine.


Tukio hilo limetokea June 19 mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri ambapo askari polisi walikutana na watu waliowatilia shaka kutokana na jinsi walivaa.


Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Kamanda wa Polisi Mkoani Mumbeya Ahmed Msangi alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa watuhumiwa hao wa ujambazi hao waliarifiwa na walinzi wa soko kuu la Tunduma.


Amesema mara baada ya kupata taarifa hizo askari waliokuwa doria walianza msako mkali wa kuwatafuta watu hao.
Amesema kutokana msako huo walifanikiwa kuwaona watu hao wawili wakiwa wamevalia makoti makubwa meusi huku mwingine akiwa amebeba mfuko mkubwa ambao ulikuwa silaha.


Kamanda Msangi amesema mara baada ya kuwaona watu hao walisimamisha ambapo walianza kukimbia na mmoja kati yao aliyekuwa amevaa jaketi jeusi alikimbia kwa umbali wa mita ishirini na kuanza kufyatua risasi hovyo huku akielekea eneo waliopo askari.


Amesema mara baada ya kuona hali hiyo askari walijibu mapigo na katika majibizano hayo ya kurushiana risasi mtuhumiwa Kapinga ambaye alikuwa akitumia bunduki aina AK.47 yenye namba 592058 na yenye risasi 25 kwenye alikufa papo hapo.


Hata hivyo Msangi amebainisha kuwa katika tukio hilo hakuna madhara kwa wananchi wala askari yaliyotokea huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuendelea kumtafuta mshukiwa mwingine.

chanzo;fahari news

Post a Comment

0 Comments