Header Ads Widget

KIJANA MWANAHARAKATI (PETRO KIMARO) AMETEULIWA KUWA KATIBU KWA TIKETI YA CHAMA CHA CHADEMA KATIKA MTAA WA KILIMANI, KATA YA MANZESE:


                                                                    Mh. Petro Kimaro
Leo katika mtandao huu wa kwetu miono umekutana na kijana mwana harakati mpya katika nyanja za siasa ambaye ameteuliwa kuwa katibu kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA katika mtaa wa kilimani huko manzese jijini dare es salaam.

Kwanza nianze kwa kumuombea dua njema, mwenyezi mungu amjaalie Hekima katika harakati zake na juhudi alizonazo katika kulikomboa taifa hili, na amjaaliwe wepesi kwa kila jambo atakaloamua liwe la heri na lenye kuleta mabadiliko katika ujenzi wa taifa.

Katika harakati zangu mimi niliamua kukutana na Kimaro na nikajaribu kumuuliza:

Ni nini malengo yako katika hili eneo?

Na majibu yake yalikuwa hivi!

Kimaro: mimi kama kijana mwana harakati ninayependa maendeleo katika taifa hili, napenda kuwaambia wana kilimani ya kuwa nitawatumikia kwa moyo mmoja, na pasipo kurudi nyuma, na pia ninachowaasa vijana wenzangu ni kwamba, wakumbuke ya kuwa ukikubali kununuliwa kwa kiasi Fulani cha fedha kutoka kwa wagombea wa uongozi katika ngazi yoyote ujue utajutia huduma pindi utakapokuwa unahitaji msaada wowote kutoka kwa huyo kiongozi aliyekurubuni kipindi cha uchaguzi!

Kwa sababu:

1. Atakuwa anahitaji kurejesha kile alichokupatia kipindi akihitaji kura yako.

2. Kama alikopa Bank atarejesha kwa njia gani kama sio kukuomba wewe rushwa?

3. Kama alinunua kura yako kwa pesa, na wewe ni lazima umnunue kwa pesa wakati wa huduma.

Nini ushauri wako kwa wanakilimani?

Kimaro: Mimi kama mwanakilimani mwenzenu, nawaasa ya kuwa msikubali kununulika kirahisi kwa maslahi ya mtu binafsi, fanyeni maamuzi, na muwachague viongozi makini na wenye uwezo wa kuongoza bila ya kuwaletea matatizo ya rushwa.

Na katika uchunguzu nilioufanya hapa maeneo ya kilimani, kuna wajumbe na wenye nyumba ambao huwalazimisha wapangaji wao kuwa na Card za vyama vyao, na hata atakayebisha, kama hatapewa Ontice, basi ujue atakuwa na vikwazo vingine . ukihitaji harakati usirudi nyuma kamwe, songa mbele.

Mungu awape hekima wanakilimani,

Nasema “CHADEMA” “AMANI KWA WOTE”

Wao watumie pesa, sisi tunatumia : “peoples! Power!”

“nitawaeleza mengi pindi tuitakapokutana kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa”

MUNGU AWABARIKI SANA.
                                                        Mh. Petro Kimaro hapo juu.

Hayo ni maneno yaliyosemwa na Mh. Katibu wa CHADEMA tawi la kilimani katika kata ya MANZESE;

Namtakia utendaji mwema katika majukumu aliyokabidhiwa:

Post a Comment

0 Comments